Monday 6th December 2021, 21:19 pm

logo

The United Republic of Tanzania

CONTRACTORS REGISTRATION BOARD

  • crblogo

KUWASILISHA FOMU ZA MREJESHO (ARF) KWA MWAKA WA FEDHA 2020/21 KWA MTANDAO

Bodi inapenda kuwataarifu Makandarasi wote nchini kwamba muda wa kuwasilisha fomu za mrejesho (ARF) kwa mwaka wa fedha 2020/21 kwa njia ya mtandao umewadia na mwisho wa kuwasilisha ni tarehe 30 Septemba 2021. Bodi haitatuma fomu za mrejesho kwenda kwa makandarasi kwa njia ya posta wala fomu hizo hazitapatikana kwa kupakua kutoka katika tovuti ya Bodi. Ili kuupata mfumo wa kukuwezesha kujaza fomu ya mrejesho mtandaoni, ingiza “URL” https://mis.crbtz.org au fuata “link” kupitia tovuti ya Bodi, www.crb.go.tz (ARF 2020/21) ili kujisajili kuwa mtumiaji wa mfumo. Kupitia mfumo wa mtandao, mtumiaji atachagua ‘‘Register ’’ ili kusajili akaunti yake ya kutumia mfumo. Mtumiaji atajaza taarifa zote zitakiwazo na kuchagua “Submit ”. Utambulisho wa mtumiaji, “username ID” na nywila, “password” vitatumwa kwa mtumiaji kupitia barua pepe iliyoingizwa na mtumiaji kipindi cha kujisajili mtandaoni. Ili kujaza fomu ya mrejesho mtandaoni, mtumiaji wa mtandao aliyejisajili ataingia mtandaoni kupitia “URL” au “link” kwa kuingiza utambulisho wa mtumiaji, “username ID” na nywila, “password” kama ilivyoelekezwa awali. Kupitia ukurasa utakaojitokeza, mtumiaji atabofya “ARF” katika “Create new ARF”’ na kuingiza taarifa zote zitakiwazo na kisha kubofya “Submit” baada ya kukamilisha. Mtumiaji atalazimika kurekebisha mapungufu hadi fomu itakapokubalika na mfumo. Uwasilishaji wa fomu hizi mtandaoni ni lazima ufanywe na Mkurugenzi Mkuu, “Managing Director” au Mkurugenzi wa Ufundi, “Technical Director”. Maelekezo haya ya jinsi ya kuufikia mfumo na kujaza fomu mtandaoni pia yanapatikana katika tovuti ya Bodi, www.crb.go.tz. Mwisho wa kuwasilisha fomu za mrejesho kwa mwaka wa fedha 2020/21 kwa mtandao ni tarehe 30 Septemba 2021.

Notice Board

Click "New" Icon Below To View Adverts

CONTRACTORS TRAINING SCHEDULE FOR FY 2021/22
KUWASILISHA FOMU ZA MREJESHO (ARF) KWA MWAKA WA FEDHA 2020/21 KWA MTANDAO
ONLINE SUBMISSION OF ANNUAL RETURN FORMS FOR THE FINANCIAL YEAR 2020/21

Video Adverts

Photo Gallery

Subscribes For Newsletter