Tuesday 6th June 2023, 21:44 pm

logo

The United Republic of Tanzania

CONTRACTORS REGISTRATION BOARD

  • crblogo

From The Press

photos are coming soon Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi. Godfrey Kasekenya amewataka Makandarasi wazawa wote nchini kuwa mabalozi wema kwa kufanya kazi nzuri zinzozingatia viwango na kukamilisha miradi kwa wakati ili Serikali ipate thamani ya fedha katika miradi yote. Agizo hilo amelitoa mkoani Mwanza akifungua mkutano wa kwanza wa Mashauriano wa Makandarasi na Wadau wa sekata ya ujenzi kwa Mwaka 2023 uliofanyika tarehe 30/03/2023 kikanda Mkoani Mwanza. “Ni muhimu kwenu Makandarasi kuzingatia uzalendo katika shughuli za kikandarasi pamoja na kutekeleza miradi kwa wakati na kwa viwango vyenye ubora kulingana na mikataba ili wanancho waweze kupata huduma bora kwa wakati na thamani ya fedha iliyokusudiwa” amesema Naibu Waziri huyo. Kasekenya amefafanua kuwa Makandarasi wana mchango mkubwa katika kuinua uchumi wa nchi yetu na endapo pale Makandarasi wanaposhindwa kutimiza wajibu wao wanawachelewesha wananchi kupata huduma zinazokuwa zimekusudiwa na pia wanaitia Serikali hasara.
Photo by:Admin, 2023-04-05 05:05:08
photos are coming soon Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) Mhandisi Rhoben Nkori ameishukuru serikali kwa kuendelea kutoa miradi mingi kwa wakandarasi wazawa ikiwemo ile ya ujenzi wa majengo ya utawala ya kiserikali, hospitali na barabara. Alisema hayo wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Bodi ya mwaka 2022 kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya pamoja na Makandarasi na Wadau wa Sekta ya Ujenzi katika ufunguzi mkutano wa kwanza wa Kikanda wa Mashauriano wa Makandarasi na Wadau wa Sekta ya Ujenzi unaofanyika jijini Mwanza tarehe 30/03/2023. Kauli mbiu ya mkutano huo ni " Kujenga Uwezo wa Makandarasi wa ndani: Mafanikio na Changamoto".
Photo by:Admin, 2023-04-05 05:04:40
photos are coming soon Msajili wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi, Mhandisi Rhoben Nkori amesema katika mkutano huo uliyofanyika kwa siku mbili 30 – 31 Machi, 2023 jijini Mwanza, wakandarasi wameweza kujadiliana mambo mbalimbali na kukubaliana hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa na Serikali. Moja ya mambo hayo ni CRB kuchukua hatua kali kwa wakandarasi wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao kwa kufuata sheria, wakandarasi wajisimamie wenyewe na wasiharibu heshima yao kwa kuruhusu watu wengine wasiokuwa makandarasi kutumia majina ya kampuni zao kupata kazi na kushindwa kufanya kazi hizo.
Photo by:Admin, 2023-04-05 05:03:46

Notice Board

Click "New" Icon Below To View Adverts

CALL FOR EXHIBITION AND SPONSORSHIP 2023
CRB EVENTS CALENDAR FOR THE FINANCIAL YEAR 2022/23
ONLINE PROJECT REGISTRATION MANUAL
PROCEDURE FOR CHANGING NAMES, SHAREHOLDERS AND DIRECTORS

Video Adverts

Photo Gallery

Subscribes For Newsletter