Tuesday 19th March 2024, 11:14 am

logo

The United Republic of Tanzania

CONTRACTORS REGISTRATION BOARD

  • crblogo

From The Press

photos are coming soon Waziri wa Ujenzi, innocent Bashungwa ameziagiza Bodi za Usajili wa Makandarasi (CRB) na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), kuhakikisha zinaandaa mpango kazi wa kusimamia na kuimarisha taaluma ya Sekta ya Ujenzi nchini ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu wake ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia. Bashungwa ameyasemaa hayo leo Tarehe 06 Novemba, 2023 jijini Dodoma, alipokuwa akizindua Bodi za ushauri za CRB na ERB ambazo zinaundwa kwa mujibu wa sheria ili kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Bodi hizo. Amesema kuwa Takwimu zinaonyesha kuwa suala la upatikanaji wa fursa nchini katika utekelezaji wa miradi kwa makandarasi wa ndani haliridhishi kutokana na kuwa licha ya makandarasi wa ndani kuwa wengi bado miradi wanayoitekeleza ni michache ukilinganisha na makandarasi wa nje. “Muandae mpango kazi wa kusaidia Makandarasi wa ndani, muujadili, kuutathmini na kuusimamia kwa pamoja badala ya kulalamika makandarasi wa ndani hawapati fursa”, amesema Bashungwa. Pia, Bashungwa amesisitiza kwa bodi hizo kuongeza ushirikiano mzuri walionao ili kusaidia taaluma hiyo kufanya kazi vizuri na kuleta maendeleo nchini.
Photo by:Admin, 2023-11-07 06:02:40
photos are coming soon Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, ameagiza Wizara kupitia Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), kuhakikisha wanakuja na mikakati ya kuwawezesha Makandarasi Wazawa kushirki katika Utekelezaji wa miradi ya Sekta ya Ujenzi nchini ili kuleta tija kwa Makandarasi hao na Taifa kwa ujumla. Ameyasema hayo Septemba 26, 2023 jijini Dodoma, wakati alipokutana na kupokea taarifa za utekelezaji wa majukumu ya Taasisi za Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Bodi ya Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) na Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC). Bashungwa ameagiza Wizara kukaa na kusikiliza changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi pamoja na kuandaa mikakati itakayosaidia makandarasi hao kutekeleza miradi mingi hasa ya kimkakati itakayoweza kuinua mitaji yao. “Linapokuja suala la ‘Local content’ yaani fursa za kiuchumi kwa watanzania, Mheshimiwa Rais kiu yake ni kuona ushiriki wa Makandarasi wazawa kwenye maendeleo ya Sekta ya Ujenzi unaongezeka”, amesema Bashungwa. Bashungwa ameeleza kuwa Takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa idadi ya Makandarasi waliosajiliwa na Bodi ni 14,550 ambapo kati ya hao 550 ni Makandarasi wa nje na 14,000 ni Makandarasi wazawa lakini katika utekelezaji wa miradi Makandarasi Wazawa wanapata asilimia 46 na Makandarasi wa nje wanapata asilimia 54. Aidha, Bashungwa ameishukuru Serikali kupitia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maboresho aliyoayaagiza katika sheria ya manunuzi kwa miradi yenye gharama ya kutoka Bilioni 10 hadi 50 kupewa kipaumbele kutekelezwa na makandarasi wazawa ili kuwajengea uwezo. Kuhusu madeni kwa Makandarasi, Waziri Bashungwa amesema kuwa kupitia Wizara ya Fedha, Serikali imeshaweka utaratibu wa kulipa madeni hayo ambapo hivi sasa kila mwezi kuanzia mwezi wa nane kiasi cha Bilioni 70 kinatengwa ambapo Bilioni 50 zinalipa madeni ya makandarasi wa ndani na Bilioni 20 ni kwa ajili ya kulipa Makandarasi wa nje. Bashungwa pia ameziagiza Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi kuhakikisha zinabuni mikakati ya kutangaza mafanikio na kazi zao kwa umma ili kuleta tija katika Taasisi hizo na Taifa kwa ujumla. Kadhalika, Bashungwa ameziagiza Taasisi hizo kusimamia wataalamu wao ili kuhakikisha wanatoa huduma sahihi na kwa wakati kwa umma na kuhakikisha wanachukua hatua kwa wale ambao watakiuka maadili ya kazi zao.
Photo by:Admin, 2023-09-27 08:34:12
photos are coming soon Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi. Godfrey Kasekenya amewataka Makandarasi wazawa wote nchini kuwa mabalozi wema kwa kufanya kazi nzuri zinzozingatia viwango na kukamilisha miradi kwa wakati ili Serikali ipate thamani ya fedha katika miradi yote. Agizo hilo amelitoa mkoani Mwanza akifungua mkutano wa kwanza wa Mashauriano wa Makandarasi na Wadau wa sekata ya ujenzi kwa Mwaka 2023 uliofanyika tarehe 30/03/2023 kikanda Mkoani Mwanza. “Ni muhimu kwenu Makandarasi kuzingatia uzalendo katika shughuli za kikandarasi pamoja na kutekeleza miradi kwa wakati na kwa viwango vyenye ubora kulingana na mikataba ili wanancho waweze kupata huduma bora kwa wakati na thamani ya fedha iliyokusudiwa” amesema Naibu Waziri huyo. Kasekenya amefafanua kuwa Makandarasi wana mchango mkubwa katika kuinua uchumi wa nchi yetu na endapo pale Makandarasi wanaposhindwa kutimiza wajibu wao wanawachelewesha wananchi kupata huduma zinazokuwa zimekusudiwa na pia wanaitia Serikali hasara.
Photo by:Admin, 2023-04-05 05:05:08

Notice Board

Click "New" Icon Below To View Adverts

BUSINESS MASTERY TRAINING
DELETION OF CONTRACTORS
CONTRACTORS REVIEW INFORMATION FORM
EVENTS CALENDAR FOR THE FINANCIAL YEAR 2023/24
ONLINE PROJECT REGISTRATION MANUAL
PROCEDURE FOR CHANGING NAMES, SHAREHOLDERS AND DIRECTORS

Video Adverts

Photo Gallery

Subscribes For Newsletter